The House of Favourite Newspapers

Wakimbizi 22 Raia wa Mali Wafariki Dunia Wakiwa kwenye Boti Kuelekea Nchini Libya

0
Miongoni mwa waliofariki ni watoto 3

JUMLA ya watu 22 waliothibitishwa kuwa ni raia wa nchi ya Mali wameripotiwa kufariki dunia baada ya kukwama baharini kutokana na kuharibika kwa Boti yao wakiwa wanahama kutoka Mali na kuingia nchini Libya.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali imesema kuwa watu 22 waliofariki ni miongoni mwa watu 83 waliokuwa wakihama kama wakimbizi kutoka nchini Mali kuelekea Libya kwa ajili ya kukimbilia barani Ulaya.

 

Miongoni mwa waliofariki ni watoto watatu (3)

 

Wizara hiyo imesema tukio limetokea Juni 22 ambapo Shirika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi pia limethibitisha kuwa jumla ya watu 61 wamefanikiwa kuokolewa katika tukio hilo huku wengi wao wakiwa na hali mbaya kiafya ambapo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Watoto watatu wametolewa wakiwa wameshafariki

Imetajwa sababu iliyopelekea vifo vya raia hao kuwa ni upungufu wa maji mwilini pamoja na kuzama.

 

Aidha kumekuwa na changamoto kubwa sana ya wakimbizi kukimbia makazi yao na kukimbilia mataifa ya Ulaya hasa nchini Hispania ambapo kwa sasa nchi ya Libya imekuwa ikitumika sana kama njia ya wakimbizi wengi kupita na kuzamia barani Ulaya.

Waokoaji wamefanikiwa kuokoa watu 61 huku 22 wakiripotwa kupoteza maisha

Tayari mataifa mengi ya Ulaya yametahadharishwa juu ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wakimmbizi kuingia katika nchi zao kutoka barani Afrika na maeneo mengine ya Bara la Asia, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ugumu wa maisha unaotokana na Janga lavita kati ya Urusi na Ukraine lakini pia madhara ya Janga la Uviko-19 ambalo limesababisha hali ngumu ya uchuni kwa mataifa mengi hasa ya Bara la Afrika.

 

Hivi karibuni kumeripotiwa tukio la watu 23 kati ya 2,000 kuuawa nchini Morocco wakati wakifanya jitihada za kuvuka mpaka wa Melilla kuingia nchini Hispania, tayari Mamlaka za Usalama za Hispania na Morocco zimeanza uchunguzi juu ya tukio hilo.

Leave A Reply