The House of Favourite Newspapers

Kidato cha Nne Waanza Mtihani wa Taifa

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne umeanza kufanyika leo nchi nzima huku kukiwa na jumla ya watahiniwa 485,866 waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2019 na kati yao wa shule ni 433,052 na 52,814 wa kujitegemea.

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa hao wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842.

 

Mwaka 2018 idadi ya watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 427,181 na hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 5,871 kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana.

 

Amewataka wasimamizi wa mitihani, wamiliki wa shule, walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani huu kwani Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha.

Comments are closed.