The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 25,000 Kuongezwa Kudhibiti Vurugu Afrika Kusini

0

SERIKALI ya Afrika Kusini inajiandaa kuwapeleka kwenye sehemu mbalimbali nchini humo wanajeshi wapatao 25,000 kwa ajili ya kudhibiti ghasia zinazoendelea kwa siku sita mfululizo.

 

Watu 72 wamekufa na wengine zaidi ya 1,200 wamekamatwa katika maandamano ya kupinga hatua ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma kufungwa miezi 15 jela.

 

Serikali imesema matukio 208 ya uporaji na uharibifu yaliripotiwa jana huku idadi ya wanajeshi waliopelekwa kudhibiti vurugu ikiongezeka mara mbili hadi 5,000.

 

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, Novisiwe Mapisa-Nqakula amewasilisha ombi bungeni la kupelekwa wanajeshi 25,000 wa ziada.

 

Hatua hiyo itahitaji kuidhinishwa na Rais Cyril Ramaphosa ambaye tayari alishaidhinisha kusambazwa wanajeshi ili kuwasaidia polisi kukabiliana na vurugu.

 

Jana Rais Ramaphosa alikutana na viongozi wa kisiasa na alielezea wasiwasi wake kwamba baadhi ya maeneo ya nchi huenda yakakosa huduma muhimu kutokana na kuharibiwa kwa mfumo wa kusambaza chakula, mafuta na dawa.

Leave A Reply