Wananchi wapongeza tamasha la EFM la ‘Mchizi wangu’

Rais wa Singeli, Suleiman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza tamashani.


Tamasha lilipambwa na burudani mbalimbali kama unavyojionea.

Amsha amsha kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakionyesha nyuso za furaha wakati wakipata burudani.

Umati wa watu ulivyofurika katika Tamasha la Mchizi Wangu Concert.
Mashabiki na wasikilizaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 Efm kilichopo kawe jijini Dar wemelipongeza Tamasha la Mchini Wangu lililofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam Februari, 14 (Siku ya Wapendanao), katika kuwapa ladha halisi ya Mtanzania .
Wananchi hao wamepongeza kwa kupata ladha ya muziki wenye asili ya Mtanzania kama vile mchiriku, singeli na nyinginezo pamoja na kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Skide mtoto wa mama Shante , Suleiman Jabir ‘Msaga Sumu’ na wengine kibao.

