The House of Favourite Newspapers

Wanaodaiwa Kumteka Mo Dewji, Kesi Yafikia Hapa – Video

0

MUSA TWALIBU mkazi wa jijini Dar es Salaam,  anayekabiliwa na kesi ya tuhuma ya kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji Mo,  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa yupo mahabusu kwa muda mrefu na jalada lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)  akitaka kujua ni kwanini halijafanyiwa maamuzi yoyote hadi leo.

 

Mshtakiwa huyo amedai hayo leo Agosti 25, 2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, akiongeza kuwa wenzake hadi leo hii hawajakamatwa.

 

Awali Wakili wa Serikali, Faraji Nguka,  amedai kuwa upelelezi umekamilika hivyo jalada lipo kwa DPP na lipo kwenye hatua ya usomaji kwa ajili ya kutolea maelekezo.

 

Hakimu Shaidi amemtaka mshtakiwa huyo amwandikie barua DPP ili atoe malalamiko hayo na yaweze kufanyiwa kazi. Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 8, mwaka huu,  litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

 

Katika kesi ya msingi washtakiwa, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wanadaiwa Oktoba 11, 2018,  maeneo ya Hoteli ya Colloseum wilayani Kinondoni Dar es Salaam, na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara Mo kwa nia ya kumhifadhi kwa siri na kumweka maeneo ambayo ni hatari.

 

Leave A Reply