The House of Favourite Newspapers

Wanasayansi wagundua chumvi Mwezini

BAHARI kubwa inayopatikana katika mwezi wa sayari ya Jupiter ina chumvi kama ile inayotumika katika sayari hii (duniani).

 

Kulingana na wanasayansi, darubini ya Hubble imekuwa ikichunguza mwezi kwa jina la Europa kwa muda mrefu sasa na imepata chumvi kama hiyo inayotumiwa katika chakula. Chumvi inayotumika katika chakula ndiyo inayozifanya bahari kuwa na maji ya chumvi.

 

Watafiti wanasema inamaanisha kwamba bahari inakabiliwa na vitendo vya tabia  ya volkano. Inafurahisha kwa sababu inaongeza fursa ya kuwepo kwa ishara za maisha ya ziada katika mwezi. Duniani maisha husemekana yalianzia katika  eneo la chini la bahari lenye maji yanayochemka.

 

Shirika la anga za juu nchini Marekani (Nasa) linakaribia kuanza uchunguzi mwezini huku ujumbe wa kwanza ukitarajiwa kuondoka 2023. Hadi kufikia wakati huo, wakati pekee ambao wanasayansi wameuona mwezi kwa karibu ni mwisho wa miaka ya 90 na mapema mwaka 2000 kupitia chombo kinachojulikana kama Galileo.

Kwa kutumia mwanga wa ‘Infrared’, wanasayansi walitafuta vipengee mbalimbali na kugundua kwamba chumvi hiyo ilipatikana hususan karibu na barafu na safu ya milima inayopita katika sakafu yake.

 

Profesa Mike Brown  kutoka Taasisi ya Teknolojia ya California, alisema: “Tumekuwa na uwezo kufanya tathmini na darubini kwa takriban miaka 20.  Ni kitu ambacho hakuna aliyefikiria kufanya.”

Pengine katika siku zijazo walimwengu watakuwa wakitumia chumvi inayotoka kwenye ulimwengu mwengine.

Comments are closed.