The House of Favourite Newspapers

Watumishi Kizimbani kwa Tuhumza za Kumteka Mwandishi – Video

 

WATUMISHI wawili wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wamendishwa kizimbani na kusomewa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha Watumishi hao ambao ni pamoja a na Afisa itifaki Swalehe Mwidadi (32) na mfanyakazi wa Masjala Amina Mshana (29) jana walimepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha kujibu shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

 

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali Sabina Silayo mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda,alidai kuwa washitakiwa hao kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa mawili. Alidai kuwa kosa la kwanza mnamo Mei 13 mwaka huu eneo la Sakina washitakiwa hao walimwibia Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Lucas Myovela simu aina ya Tekno C7 ya thamani ya Sh.300,000, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh.50,000 na walitumia unyangā€¯anyi huo kwa kutumia panga na mkanda wa plastiki.

 

Aliendelea kutaja kuwa vitu vingine walivyoiba ni pamoja na fedha taslimu Sh.75,000 na walijihamishia fedha Sh.9,500 za Mpesa na kadi ya ATM ya benki ya CRDB, huku wakijuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Silayo alidai kuwa kosa la pili washitakiwa wanashitakiwa kuwa mnamo Mei 13 mwaka huu,eneo la Sakina kwa pamoja walifanya kitenfo cha ukatili na udhalilishaji kwa kumvua Lucas Myovela nguo zake na kumchukua picha akiwa uchi.

 

Alidai kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kufunguliwa kesi hiyo namba 153/2018. Washitakiwa walikana mashitaka hayo na Wakili Silayo alidai upelelezi haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu Kisinda alidai kesi hiyo haina dhamana na shitaka la kwanza halina dhamana hivyo alipanga kutajwa tena Juni 5 mwaka huu.

SHUHUDIA TUKIO HILO MAHAKAMANI

Comments are closed.