The House of Favourite Newspapers

WASANII KUNUFAIKA NA VIWANJA DAR, PWANI!

KAMPUNI ya KC Land Development imesema imejipanga ili kuweza kuwasaidia wananchi wa hali ya chini viwanja vya bei rahisi ambapo kwa kuanzia, watawapa wasanii mbalimbali ili wawe mfano.

Akizungumza na Global Publishers leo jijini Dar, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Khalid Mwinyi alisema kampuni yao itatoa viwanja hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli.

“Kwa sasa tutaanza kwa kwa Mkoa wa Dar, na mikoa ya Pwani na malipo ya viwanja hivi yatakuwa ni taratibu kwa takriban miaka miwili na kwa sasa tunawaahidi kuwapatia wasanii ambao ni wanachama wa uzalendo kwanza kwa ajili ya kumiliki ardhi na kupata makazi yake,” alisema.

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Uzalendo Kwanza, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameshukuru kampuni hiyo kwa kuwaona kwenye jambo hilo muhimu na kuwapa kipaumbele.

“Ni kweli wasanii tumekuwa tukitangatanga katika nyumba za kupanga tunashukuru KC kwa kutuona na kutuwezesha kupata ardhi kwa kwa heshima ni kuwa na nyumba na si gari, maisha ni nyumba,” alisema Nyerere.

Stori: Neema Adrian

Comments are closed.