The House of Favourite Newspapers

Mastaa Wafunguka Ruge, Makonda Kupatana!

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

MWISHONI mwa wiki iliyopita, Rais Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiwa mkoani Tanga kwenye hafla ya uzinduzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda, alifanya tukio la aina yake lililowaacha wengi midomo wazi, baada ya kuwaita jukwaani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwata washikane mikono na kumaliza bifu lao.

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas `Lulu Diva’.

Hilo lilikuja baada ya Machi, mwaka huu uongozi wa Clouds kumtuhumu Makonda kuvamia kituo chao cha redio na televisheni akiwa ameambatana na polisi wapatao nane, wengi wao wakiwa na silaha za moto ambapo taarifa hizo zilieleza kuwa, alivamia ofisi hizo usiku na kutoa vitisho kwa watangazaji wa Kipindi cha Shilawadu.

Mara baada ya tukio hilo, Ruge, sambamba na Jukwaa la Wahariri waliazimia kutompa ushirikiano Makonda mpaka pale atakapoomba radhi hivyo kitendo cha Rais Magufuli kuwapatanisha, kiliamsha hisia tofauti na hapa baadhi ya mastaa Bongo wanafunguka;

Mkongwe wa filamu na tamthiliya za Kibongo, Tuesday Kihangala ‘Chuz’.

 

TUESDAY KIHANGALA ‘CHUZ’:

“Pongezi nyingi sana kwa rais kwa kujua umuhimu wa hili, pia pongezi kwa Ruge na Makonda kwa kuwa tayari kupatana ili tujenge nchi kwa pamoja.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’:

“Naona ni sawa, maana wote kazi zao zinalandana na zinahitaji washirikiane hivyo ni jambo jema, bora juhudi za kuendeleza jiji (Dar) ziendelee kwa ushirikiano, bifu hazina maana.”

Staa wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ .

ISABELA MPANDA ‘BELLA’:

“Jamani hivi ishu muhimu ya bomba la mafuta kutoa ajira za kudumu kwa Watanzania 1,500 na za muda mfupi 20,000 kwa mujibu wa JPM watu waliona siyo habari hadi wakomalie ishu ya Ruge na Makonda? Watu wameshapatana, Wabongo badilikeni.”

DAUDI MICHAEL ‘DUMA’:

“Ni kitu kizuri ili kusogeza mbele maendeleo ya nchi yetu na siyo hao tu, ningeshauri wote wenye mabifu, waweke pembeni tofauti zao tujenge taifa letu kwa umoja kwa sababu haliwezi kujengwa na mtu mmoja, ushirikiano ni lazima.”

 

BABY MADAHA:

“Ni jambo zuri, hakuna sababu ya kuwa na uadui, maisha yenyewe ni mafupi, lengo ni moja tu, kuijenga Tanzania mpya, bifu liwepo ili iweje? Ninawapongeza wote kwani ni wadau wakubwa wa sanaa.”

LULU ABBAS `LULU DIVA’:

“Jambo alilofanya rais ni ni jema sana, nimelipenda, niwatakie kila la heri.”

Leave A Reply