The House of Favourite Newspapers

WASHINDI SPOTI HAUSI WAJINYAKULIA ZAWADI ZAO KUTOKA TECNO – VIDEO

Juma Lukandila (kushoto) akikabidhiwa jezi kwa niaba ya Deogtratia Kaji wa Mwanza. Anayekabidhi jezi ni Mtangazaji wa Spoti Hausi, Elius Kambili.

 

KIPINDI bora na maarufu cha michezo kinachorushwa kila Alhamisi saa 10:00 kupitia YouTube Channel ya Global TV Onlione, SpotiHausi leo Machi 1, 2018 kimetoa zawadi kabambe kwa washindi wa shindano maalum linaloendeshwa na kipindi hicho.

 

SpotiHausi kinachodhaminiwa na Kampuni ya TECNO Mobile Limited kimetoa zawadi ya jezi ya Manchester City vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa Deogtratia Kaji wa Mwanza ambaye alichukuliwa zawadi na ndugu yake Juma Lukandila mkazi wa Tabata Dar es Salaam, zawadi ya mpira wa Mancity – TECNO ilikwenda kwa Katunzi Lueza mkazi wa Mtwara ambaye zawadi yake alichukuliwa na nduguye, Rose Maro.

 

 

Rose Maro (kushoto) akikabidhiwa mpira wa TECNO-Man City kwa niaba ya Katunzi Lueza wa Mtwara. Anayekabidhi jezi ni Mtangazaji wa Spoti Hausi, Wilbert Molandi.

 

Baada ya kukabidhiwa zawadi hizo washindi walikuwa na haya ya kunena:

Juma Lukandila mwakilishi wa Deogtratia Kaji;

“Nimefurahi sana kwa ndugu yangu kushinda hii zawadi, najisikia faraja kubwa. Kwa zawadi hii amenihamasisha nishiriki mpaka niipate simu mpya na zawadi nyingine mnazotoa kupitia Spoti Hausi.”

 

Rose Maro mwakilishi wa Katunzi Lueza;

“Nawapongeza kwa kuendesha kipindi vizuri, mwanzoni nilidhani labda ni uongo kumbe ni kweli mnatoa zawadi tena bila kumpendelea mtu. Hapa Global hatumjui mtu yeyote lakini kupitia ushiriki tu zawadi hii ameshinda ndugu yangu tena yupo mkoani. Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, nawashauri na Watanzania wenzangu watazame vipindi vya Global TV Online kila mara, kwa sababu mbali na kupata habari kuna fursa nyingine ya zawadi ambayo mtu akishinda inaweza kumsaidia kwa namna moja ama nyingine.”

 

Mbali na jezi na mpira, Spoti Hausi wiki ijayo kupitia kipindi chake itatoa zawadi ya simu mpya ya aina ya TECNO Camon CM (smartphone). Unachotakiwa kufanya ni kutazama kipindi kikiwa LIVE kila Alhamisi saa 10:00 jioni, like, comment na shere kisha unaandika namba yako ya simu.

 

SPOTI HAUSI: YANGA IKIFUNGWA INABAKI CAF, SIMBA BYEBYE

Comments are closed.