The House of Favourite Newspapers

Washindi Tusua Maisha na Global Wafunguka ya Moyoni

WASHINDI mbalimbali wa wiki iliyopita wa promosheni ya kwanza ya Tusua Maisha na Global inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, wameibuka na kufunguka jinsi walivyopokea baada ya kutangazwa washindi wa promo hiyo.

Washindi hao ni Novat Magere wa Mdaula, Pwani aliyeshinda zawadi ya jezi, Shaban Kamoye wa Manzese jijini Dar aliyejishindia dinner set, Richard Tanganyika wa Mdaula, Pwani aliyejishindia zawadi ya pikipiki na Nassor Juma aliyeshinda headphone za Beats By Dre.

Wakizungumza na Championi Jumatatu, kwa nyakati tofauti washindi hao walisema walipokea kwa furaha baada ya kutangazwa washindi wa promosheni hiyo.

 

Novat Magere kwake yeye alisema: “Kwangu ninajisikia furaha sana kwani ndiyo mara yangu ya kwanza kushiriki promosheni za Global na imekuwa bahati kwangu nimefanikiwa kushinda zawadi.

“Ninawaomba wasomaji wengine waendelee kununua magazeti ya Global na waamini kwamba hii ni kweli kabisa na hakuna ujanja wowote ambao unafanyika, mimi ni msomaji mzuri wa magazeti ya Amani na Ijumaa Wikienda,” alisema Magere ambaye anafanya biashara ya samaki mkoani Pwani.

 

Kwa upande wake, Shaban Kamoye ambaye anajishughulisha na biashara ndogondogo Manzese jijini Dar alisema: “Kwangu nilipokea vizuri sana taarifa ya kuambiwa mimi ni mshindi, nimefurahia kwamba nimekuwa mmoja wa washindi wa promo hii kwa safari hii.”

Richard Tanganyika ambaye yeye amejishindia pikipiki amesema: “Hii siyo mara yangu ya kwanza kushiriki katika mashindano ya namna hii. Nilishiriki Shinda Nyumba ile ya kwanza na ya pili na kote sikufanikiwa lakini sikukata tamaa na hatimaye nimekuwa mshindi kwa safari hii.

 

“Neno langu kwa Watanzania ni kuendelea kununua na kusoma magazeti ya Global kwani watajishindia siku moja na waamini kabisa kwamba Global wanafanya kazi yao kwa ukamilifu bila ya kuwepo kwa udanganyifu wowote pale mtu anaposhinda. Mimi nimekuwa mpenzi mkubwa wa magazeti ya Championi, Uwazi na Risasi ambapo ninanunua kila yanapotoka.

“Zawadi hii ya pikipiki itanitoa sehemu moja ya maisha yangu na kunipeleka katika ngazi nyingine, niwashukuru sana Global kwa kufanya vitu kama hivi,” alisema Richard.

 

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, amesema licha ya zawadi hizo za promosheni ya kwanza kutolewa lakini wasomaji waendelee kushiriki kutokana na kuwepo kwa zawadi kwa wiki 11.

Kushiriki promosheni ya Tusua Maisha na Global msomaji anatakiwa kununua gazeti lolote kati ya Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili utakapokutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Mwandishi wet, Dar es Salaam

Comments are closed.