The House of Favourite Newspapers

Washindi ‘Toka na Mike’ Wapatikana Dar Live, Walamba Ajira (Picha + Video)

Miongozi wa washiriki  30 wa shindano la utangazaji walioingia fainali.
Katibu Mkuu wa  Baraza la Sanaa nchini (Basata) Geofrey Mungereza,  akitangaza washindi.
Geoffrey Pangapanga akilia kwa furaha baada ya kupita kwenye fainali hiyo.
Watangazaji wapya watatu waliowabwaga wenzao kwenye fainali hiyo na kulamba ajira. Kutoka kushoto ni Geoffrey Pangapanga, Mina Billia na Ramadhani Tembo.
Washindi wakipewa ving’amuzi  na madishi ya DSTV.

KINYANG’ANYIRO cha kutafuta watangazaji bora kilichofanyika katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem, jijini Dar es Salaam, kiliisha kwa kuwaibua washindi watatu ambao waliingia mkataba wa kudumu wa kuitumikia Radio Times FM, ambao ni: Ramadhani Tembo wa Dar, Amina Bilia wa Mbeya na Geofrey Pangapanga.

Washindi hao walitangazwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa (Basata) Geofrey Mungereza, aliyekuwa mgeni rasmi.

Baada ya watangazaji hao wapya kujitwalia ajira hizo Khadija Kopa, Barnabas na wasanii wengine waliendeleza burudani mpaka majogoo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.