The House of Favourite Newspapers

Watoto Huwaambii Kitu JUICE KINGDOM

SIKU chache baada ya kuzinduliwa vinywaji vya Juice Kingdom tawi la Tabata-Segerea, taarifa ni kwamba vinywaji hivyo vimependwa sana na watoto ambao wameonja baada ya kupelekwa na wazazi wao.

 

Tawi hilo la Juice Kingdom lilizinduliwa Septemba 14, mwaka huu ambapo watoto walifurika na kuonja ladha mbalimbali za juisi hizo ambazo zinatengenezwa na matunda halisi bila kuongeza kemikali ya aina yoyote.

Mmoja wa wazazi ambao walifika eneo hilo, John Kiketo, alisema kiwanja hicho kimekuwa ‘cha nyumbani’ kwa sasa kwani mbali na wanawe kufuata juisi, yeye anaburudika kwa vyakula na vinywaji vingine vinavyopatikana hapo.

“Wanangu na mke wangu wao wanapenda juisi, mimi nakunywa bia sasa bahati nzuri hapa wameweka na bia hivyo kila wikiendi lazima tufike hapa.

 

“Watoto wangu pia huwa wanapenda baga ambazo tunazipata hapahapa kwa hiyo kila kitu tunapata hapa,” alisema John.

 

Kwenye uzinduzi wa Juice Kingdom, mbali na watu kufurahia juisi pamoja na vyakula, siku hiyo watu waliweza kupata nafasi ya kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva na Bongo Movies.

 

Kwa upande wa Bongo Movies, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ waliweza ‘ku-show love’ na mashabiki wao huku wakinywa juisi mbalimbali za Kingdom.

 

“Ni juisi ambazo kwa kweli sijawahi ona mahali popote Bongo. Sisi tunakunywa juisi mbalimbali lakini hii ni tamu, haichoshi tangu nimefika hapa nakunywa tu,” alisema Johari.

 

Wasanii wa Bongo Fleva waliotumbuiza siku hiyo na kupata shangwe kubwa ni pamoja na Young D, Dogo Janja na Q Boy Msafi.

Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron Julius alisema burudani kwa upande wa Tabata-Segerea ndio kwanza inaanza hivyo mashabiki wanaopenda vitu vyenye ubora wafike stendi ya Segerea kuburudika.

Alisema, tofauti na matawi yake mengine yaliyopo katika kona mbalimbali jijini Dar, tawi hilo la Tabata-Segerea lina nyama choma, baga, kuku na vyakula mbalimbali pamoja na bia!

Comments are closed.