The House of Favourite Newspapers

Watoto Wawili Wafariki Baada Ya Nyumba Kuungua Kwa Moto Kagera

Watoto wawili wa kike, mmoja wa mika miwili na mwingine wa miezi 6 wamefariki dunia  usiku wa kuamkia leo baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.

 

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni kibatari kilichokuwa kikiwaka, kuangukia godoro na chandarua.

Taarifa z kuwa wakati moto huo unaanza, mama wa watoto hao alikuwa amekwenda kwa jirani kuomba chumvi.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi amesema amepokea taarifa hizo na akatoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari.

Comments are closed.