The House of Favourite Newspapers

WATUMISHI FANYENI KAZI KWA UHAKIKA NA MJIAMINI-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabulla wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kuanza ziara ya mkoa huo, Februari 15, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege  wa Mwanza kuanza ziara ya kazi mkoani humo Februari 15, 2018. 
tttWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na viongozi wa serikali, Vyama vya Siasa na viongozi wa dini kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kuwasili  na kuanza ziara ya kikazi mkoani humo Februari 15, 2018.  Watano kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

 

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma watumie utalaamu wao vizuri na wafanye kazi kwa uhakika na kwa kujiamini ili  matokeo ya utendaji wao yaonekane.

 

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Februari 15, 2018) mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza alipowasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku saba.

 

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa watumie utalaamu wao vizuri na wafanyekazi kwa kujiamini pamoja na kuwa na taarifa za kutosha za idara wanazoziongoza ili wananchi waweze kupata tija.

 

Pia amewataka watendaji kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika ipasavyo.

 

“Msimamo wa  Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe na vitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”

 

Pia Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

 

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongela alimueleza Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanafanya kazi kwa bidii na fedha zote za miradi zinatumika kama ilivyokusudiwa.

 

Hata hivyo Bw. Mongela alizungumza kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika mkoa huo kuwa ni ya kuridhisha na imefikia asilimia 80, pia wameboresha huduma ya mama na mtoto.

 

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Comments are closed.