The House of Favourite Newspapers

WAZIRI AHIMIZA UPENDO KWA WAKULIMA, WAFUGAJI MKURANGA

0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ullega akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Nyanduturu kata ya Nyamato Wilaya ya Mkuranga.
Abdallah Ulega Akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Tipo.
Ullega akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Tipo wilayani Mkuranga muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wake.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ally Mohamed akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Ullega akiwa katika jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kifumangao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ullega akiteta jambo na baadhi ya wananchi wa kabila la wamasai.
Mmoja wa akina mama katika moja ya vijiji alivyovitembelea akiuliza swali.
Mzee wa Kijiji cha Tipo akiuliza swali kwa waziri huyo.

 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ullega amewataka wakulima na wafugaji waondokane na chuki iliyopo kati yao ikiwa ni njia ya kuboresha amani na mshikamano.

 

Katika ziara yake akiwahutubia wananchi wa Mkuranga jana, Ullega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga (CCM), alisema hakuna jambo baya katika maisha kama kucheza na amani, kwani ikishapotea kuirejesha huwa ni kazi ngumu.

 

Aidha, Ullega alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi ya Naibu Waziri na kuahidi ataitumikia vyema nafasi hiyo kama ilivyoelekezwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu.

 

“Ndugu zangu, mimi ni mtumishi wenu na taifa kwa ujumla hivyo naahidi kuwa nanyi bega kwa bega katika kuhakikisha tunasongesha pamoja gurudumu la maendeleo, lakini muhimu sana nataka niwasihi kuondoa tofauti zenu, chuki hazina maana yoyote, wakulima na wafugaji pendaneni, sisi sote ni Watanzania, tunajenga taifa moja kwa nini tugombee fito?

 

“Hakuna kitu kibaya kama kuchezea amani, ikiondoka kuirejesha huwa ni vigumu, ndugu zangu bila upendo hakuna maendeleo yanayoweza kufanyika.

Kwa sasa ni vyema kama mkatengeneza vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ikiwemo mifugo nami kwa nafasi yangu kama mbunge na naibu waziri wa wizara husika nitashirikiana nanyi,” alisema Ullega.

 

Hata hivyo, mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwasilisha kero zao ambapo walifanya hivyo na yeye kuahidi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo, pia alichangia ujenzi wa zahanati katika vijiji vya Kifumangao, Tipo, Nyamato na Nyanduturu ambapo alitoa mifuko 200 ya saruji na pesa kiasi cha shilingi millioni 6 kama sehemu ya ukamilishaji wa ujenzi huo.

 

vijiji vinne alivyotembelewa wa Wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane

 

Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.

 

Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply