The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu wa Israel Aachia Madaraka, Netanyahu Ajipanga Kurudi Madarakani

0
Waziri Mkuu Mpya wa Israel Yair Lapid akiwa na Waziri Mkuu aliyeachia Madaraka Naftali Bennett

ISRAEL imemtangaza Yair Lapid kama Waziri Mkuu mpya wan chi hiyo akichukua nafasi ya Waziri Mkuu Naftali Bennett aliyakaa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

 

Lapid ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Centrist ataliongoza Taifa hilo hadi kufikia Uchaguzi Mkuu wa Novemba 1.

 

Lapid anajiandaa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu alipania kurudi tena madarakani.

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Benjamin Netanyahu

Naftali Bennett alikabidhi madaraka kwa Lapid siku ya Alhamis kama yalivyo makubaliano ya kubadilishana madaraka ya Uwaziri Mkuu, ingawa Bennett amebainisha kuwa hatagombea tena uchaguzi wa mwezi Novemba.

 

Waziri wa zamani wa nchi hiyo na Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu Benjamin Netanyahu amepongeza hatua hiyo akidai kuwa ni hatua muhimu sana kwa maendeleo ya siasa na demokrasia ya Taifa la Israel.

Leave A Reply