The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu wa Uingereza Alaani Ubaguzi wa Rangi

0

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelaani ubaguzi wa rangi uliojitokeza katika mitandao ya kijamii dhidi ya wachezaji wa England baada ya timu hiyo kushindwa na Italia katika fainali ya kuwania kombe la Euro 2020.

 

Polisi nchini Uingereza imesema itachunguza matusi na maneno ya ubaguzi wa rangi yaliyoandikwa katika mitandao ya kijamii dhidi ya wachezaji watatu wa England waliolengwa kwenye kadhia hiyo ambao wana asili ya Afrika Marcus Rashford, Jardon Sancho na Bukayo Saka.

 

Wachezaji hao walipoteza mikwaju ya penalti baada ya Italia na England kutoka sare bao 1-1 usiku wa kuamkia leo, mechi iliyochezwa katika uwanja wa Wembley mjini London mbele ya mashabiki 60,000 wengi wakiwa wanashabikia England. Kupitia mikwaju hiyo ya penalti Italia iliibuka na ushindi kwa mabao 3-2.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Boris Johnson amesema timu ya taifa England yapaswa kusifiwa kama mashujaa na si kutupiwa kauli za ubaguzi wa rangi. Johnson ameongeza kuwa waliohusika kwa ubaguzi huo wa kushangaza wanapswa kuona aibu wenyewe.

 

Leave A Reply