The House of Favourite Newspapers

Waziri Shonza Ampa za Chembe Sister Fey

NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amempa za chembe msanii wa Bongo Fleva, Faidha Omary ‘Sister Fey’ kwa kutumia nguvu nyingi kutengeneza kiki badala ya kuonesha uwezo wa kazi.

 

Shonza alisema hayo usiku wa kuamkia jana alipohudhuria uzinduzi wa mpango wa mwigizaji mkongwe wa sinema za Kibongo, Yvone- Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ wa kuinua vipaji vya filamu kwa wasichana uitwao Mona ACT uliofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.

 

Katika uzinduzi huo, wasichana 50 ambao walichujwa kutoka katika kundi la wasichana 500 walionesha umahiri mkubwa wa kuigiza ndipo Shonza akaanza kuwamwagia sifa. Shonza alisema msanii anatakiwa apate umaarufu kupitia kazi yake na siyo kiki.

 

“Msanii wa kweli ni yule anayejipatia umaarufu kupitia kazi yake na siyo kiki, ukifanya kazi nzuri utapata umaarufu bila hata kiki. Sasa mtu kama Fey mimi siwezi kumuita msanii, inabidi umaarufu uupatie kwenye kazi siyo kiki kila kukicha,” alisema Shonza.

Shonza aliwasihi wasichana hao kutafuta umaarufu kupitia vipaji vya sanaa na kuachana na kiki zisizokuwa na maana.

STORI: Richard Bukos, DAR

INASIKITISHA! Afungiwa Bandani Zaidi ya Mwaka, Maisha yake ni Hatari!

Comments are closed.