The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Akanusha Tuhuma za Rais Putin Kuwa Mgonjwa

0
Rais wa Urusi Vladimir Putin

KWENYE kipindi cha mahojiano alichofanya na Televisheni ya Ufaransa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amekanusha tuhuma na taarifa zinazosambaa kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ni mgonjwa.

 

Kumekuwa na uvumi wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani kuwa Rais Putin anaweza kuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo yawezekena ikawa ni saratani.

 

Mahojiano hayo yamefanyika wakati ambao Urusi inaendelea na vita nchini Ukraine katika jimbo la Donbas.

 

Lavrov alinukuliwa akisema:

“Ukombozi katika eneo la Donbas ilikuwa ni kipaumbele kikubwa.”

 

“Sidhani kama watu wanaweza wakaona ishara yoyote ya ugonjwa kwa Rais Putin, unaweza ukamtazama kwenye Luninga, soma na sikiliza hotuba zake, kwa sasa nawaachia hao wanaosambaza taarifa za uongo achilia mbali hali halisi anayoonekana nayo Rais Putin katika hadhara.”

Mapigano makali yanaendelea katika Jimbo la Donbas kati ya Urusi na Ukraine

Vyanzo vya kiintelijensia vya Serikali ya Uingereza vilinukuliwa vikiliambia Shirika la Utangazaji la nchi hiyo BBC kuwa hali ya Rais Putin ilikuwa dhoofu wiki iliyopita utokana na kile kinachosadikika kuwa ni kusumbuliwa na maradhi ya saratani.

Taasisi za kiintelijensia za nchi za magharibi zimekuwa zikifuatilia kwa ukaribu sana hali ya kiafya ya Rais Putin.

Leave A Reply