The House of Favourite Newspapers

WEMA: AUNT HAJAWAHI KUNICHOKA

Wema Sepetu na Aunt Ezekiel

STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa pamoja na mambo mengi ambayo yamekuwa yakimtokea, rafiki yake wa kweli ni  Aunt Ezekiel kwani hajawahi kumchoka na kumtenga kama wafanyavyo wengine.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wema alisema kuwa ana marafiki wengi lakini baadhi ni wanafiki ila Aunt ana upendo wa kweli kwake. “Nimegundua kuwa rafiki wa kweli kwangu ni Aunt, amenipa faraja ya kweli kipindi chote cha matatizo, naamini ana upendo na mimi,”alisema Wema.

STORI: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.