WEMA YUPI UNATAMANI AWE WEMA WA LEO?

MWAKA 2006 alipoibuka kidedea kwenye mashindano ya Miss Tanzania, hapo ndipo mwanadada Wema Isack Sepetu ‘Madam’ alipoanza kung’ara. Wakati huo akiwa bado mbichimbichi, Wema alikuwa Wema kwelikweli. 

 

Hapa nazungumzia muonekano wake kwani alikuwa binti mrembo, aliyekwenda hewani na shepu yake ilikuwa namba nane, ngozi yake ilikuwa orijino na ukichanganya na kale kasauti kake ka’ kitoto, hakuna mwanaume ambaye hakutamani awe wake. Kwa kifupi Wema wa kipindi kile alikuwa zaidi ya mrembo na hicho ndicho kilichomfungulia njia kuelekea kwenye umaarufu ambao sasa hivi ni kama unasinyaa hivi.

 

Kwa wanaokumbuka, Wema alizidi kuwa gumzo baada ya kujiingiza kwenye masuala ya uigizaji wa filamu kisha kujiweka kimapenzi kwa msanii wa filamu ambaye kwa sasa ni marehemu, Steven Kanumba. Safari yake ya kimapenzi haina nafasi katika makala haya ya leo lakini nataka tu umkumbuke yule Wema wa kipindi kile kabla hajachanganya kwenye mambo ya filamu. (Angalia picha namba moja).

Baada ya hapo kuna Wema ambaye aliibuka mwenye muonekano mwingine kabisa. Huyu ni Wema ‘bonge nyanya’ ama Wema tipwatipwa. Kwa wanaomfuatilia staa huyu watakumbuka kuna wakati alinenepa hadi watu wakahoji kulikoni? Alikuja na figa ambayo nayo iliwavutia wengi hasa wanaume ambao ni wagonjwa wa misambwanda.

 

Lile umbo lake namba nane lilibaki vilevile lakini sasa, makalio yake yaliongezeka kwa kiwango kikubwa sana. Wapo waliosema kalio lile lilikuwa ni la kurithi kutoka kwa mama yake, Miriam Sepetu maana naye si haba lakini wapo waliokwenda mbele zaidi na kusema eti alikuwa akijaladia.  

Nakumbuka iliwahi kuelezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, eti staa huyo alikuwa akivaa zile taiti za sponji ambazo ndizo zilizokuwa zikimtunisha makalio yake. Ukiacha hao waliokuwa wakisema hivyo, wapo ambao walikwenda mbele zaidi na kudai Wema alikuwa akitumia dawa za Kichina za kuumusha makalio. Kwa kifupi kila mmoja alisema lake kutokana na shepu lile lakini ukweli alikuwa akiujua Wema mwenyewe na watu wake wa karibu.

Lakini mbali na maneno yote hayo, wengi walitokea kuipenda shepu ile na wapo wasichana waliokuwa wakiuliza wafanyeje ili wawe kama Wema. Watu hao ilikuwa ngumu kuwashauri kwa kuwa shepu ya mtu inatokana na alivyoumbwa na Mungu, sasa kama kuna mambo mengine ya kulitengeneza shepu feki, hilo ni suala la mtu husika kujiongeza.

 

Kwa maana hiyo sasa, muonekano wa pili wa Wema ambao uliwashika watu ni huo wa shepu tipwatipwa. Angalia picha namba mbili. Baada ya mrembo huyo kutikisa kwa muda mrefu na shepu yake hiyo, kuna wakati hapo katikati akapatwa na misala mbalimbali ambayo kimsingi ilimchanganya sana. Akapotea kwa kipindi kirefu na waliokuwa wakimuona walieleza kuwa, Wema alikuwa amekonda sana hadi anatia huruma.

Ilikuwa ngumu kuelewa kukonda huko kulikuwa kwa namna gani hadi atie huruma? Hapo ndipo wengi walipokuwa wakitamani kumuona. Na kweli haikuchukua muda mrefu akaanza kuachia picha moja baada ya nyingine akiwa amerudi utotoni.

 

Yaani hakuwa Wema yule ambaye akifika maeneo, lazima watu washituke. Msambwanda wote ukawa umeyeyuka na kuwafanya watu waongee hata yale wasiyo na uhakika nayo. Kuna waliosema kajikondesha makusudi na kuna waliosema matatizo yaliyompata ndiyo yaliyochangia lakini wengine wakaenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, alikuwa akiumwa.

Kwa kweli muonekano huu mpya wa Wema haujawavutia wengi licha kuwepo kwa baadhi ya wanaosema ni bora amepungua maana unene wake haukuwa wa afya. Yote kwa yote, Wema ni Wema. Sasa wewe msomaji ukipewa nafasi ya kuchagua Wema yupi awe wa sasa utamchagua yupi?

Jibu lako nitumie kwenye namba 0658798787.

 

MAKALA: AMRAN KAIMA

Loading...

Toa comment