The House of Favourite Newspapers

Werrason kukinukisha Dar Jumamosi hii

Werrason akiwasili fukwe za Escape One na wanamuziki wenzake huku akiongozwa na mwenyeji wao ambaye ni mtangazaji wa Clouds FM, Hamisi Dakota.
Werrason akizungumza mbele ya waandishi wa habari.

MSANII wa muziki wa dansi kutoka  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Werrason yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya shoo Jumamosi hii katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Muda mfupi uliopita mwanamuziki huyo alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika fukwe hizo ambapo amesema hapa nchini anamfahamu Msanii Diamond Platnumz pekee maana amekuwa akimsikia mara kadhaa akitajwa huko Congo.

Werrason na wanamuziki wake wakitoa kionjo cha wimbo kabla ya kuhitimisha kikao na wanahabari.

Hivyo amewaomba wasanii wa hapa nchini  wamtafute kuanzia leo ili wabadilishane mawazo na hata ikiwezekana kufanya klabo ya pamoja kabla ya siku yake ya kufanya shoo yake hiyo ya Jumamosi na ile ya Jumanne katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali ya kikao hicho kilichofanyika katika fukwe za Escape One mapema leo.

“Waafrika ni kitu kimoja hivyo ningependa wiki hii moja ambayo nipo hapa nipate kubadilishana mawazo na wasanii wa hapa Tanzania, ila hata kama kuna mtu angependa tufanye ngoma ya pamoja nipo tayari kwani kufanya hivyo ni kukuza muziki wetu wa Afrika ambapo utapata promo ya nchi nyingi jirani,” alisema Werrason.

HABARI,PICHA:MUSA MATEJA,GPL.

 

Comments are closed.