The House of Favourite Newspapers

Winga Mcongo azuiwa mazoezini Yanga

KATIKA hali ya kushangaza, juzi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alimzuia kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ruben Bomba kukanyaga kwenye mazoezi ya timu hiyo.

 

Bomba, raia wa DR Congo, anayetokea kwenye akademi ya Azizi Makukula, aliyechezea timu ya taifa ya Ureno, yupo nchini kwa ajili ya kujiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo utakaofungwa Desemba 15, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera (pichani) alisema kuwa licha ya mchezaji huyo kufanya mazoezi siku moja, lakini aliamua kumsimamisha kwa kuwa hakutaka kuvuruga mipango yake.

“Bomba amefanya mazoezi na sisi siku moja ya Ijumaa lakini leo (juzi) hakuweza kufanya kwa sababu nilizuia yeye kuja mazoezini kwa kuwa hakuwa kwenye mipango ya mechi yetu na Biashara United.

 

“Unajua bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi halafu wakati anakuja sisi tulienda Mbeya, hivyo hata mazoezi ya siku moja aliyofanya hayawezi kutoa ubora wake na tulifanya sana fiziki kuliko kuchezea mpira ila mazoezi yanayofuata atakuwepo,” alisema Zahera.

 IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam.

MASHINE MPYA ILIYOSAJILIWA YANGA HII HAPA TAIFA – VIDEO

Comments are closed.