The House of Favourite Newspapers

Wizkid Azidi Kuwaburuza Davido, Diamond iTune

MSANII kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim ‘Wizkid’ amezidi kuwakimbiza wasanii wa Afro Pop kwa Bara la Afrika akitajwa kuwa ni msanii wa 77 kwenye orodha ya wasanii wanaosikilizwa kwenye Spotify (Most Streamed Artist) na kushikilia nafasi ya 315 kwenye orodha ya wasanii wanaofanya vizuri kwa mauzo kwenye mtandao wa iTunes duniani kwenye Global Digital Artist Ranking ya leo Novemba 3, 2018.

 

Hasimu wake, David Adedeji Adeleke ‘Davido’ ametajwa kuwa ni msanii wa 513 kwenye orodha ya iTunes duniani huku Mtanzania, Naseeb Abdul Juma, ‘Diamond Platnumz’ akishika nafasi ya 2749. Ikumbukwe kwamba, Fally Ipupa ambaye anafanya mziki wa Dansi kutoka Kongo DR, ndiye anaongoza kwa ujumla Barani Afrika akishika nafasi ya 312 duniani.

 

 

Comments are closed.