The House of Favourite Newspapers

Wolper Adai Hawezi Kucheat, Awataka Mashabiki Kusubiri Kazi Inayoshirikisha Mastaa

0
                   Mwanadada Wolper ambaye ni Muigizaji wa Bongo Muvi

NYOTA wa Bongo Muvi Wolper amedai kuwa yeye hawezi kudanganya (kucheat) iwe katika mahusiano au katika mambo mengine ya msingi kama vile biashara au kazi.

 

Akiongea na Global TV wakati anaelezea mikakati mbalimbali ya kazi zake za uigizaji amesema hawezi kufanya kazi za kuajiriwa zaidi ya moja kwani hawezi kujigawa ni vema afanye kazi yake binafsi na angalau moja ya kuajiriwa.

                                                          Wolper akiwa na mpenzi wake kwenye gari

“Unajua kiukweli mimi siwezi kucheat kama ilivyo kwenye mahusiano, yaani siwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja sawa napenda sana hela lakini siwezi kufanya huku na kule naweza kuwaharibia watu kazi zao.”

 

Sambamba na kuzungumzia mikakati yake lakini pia amesema mashabiki wa Bongo Muvi wategemee kazi nzuri na muda si mrefu yeye na waigizaji wenzake wataweka wazi kazi yao mpya kupitia mkutano na waandishi wa habari.

 

Wolper ameendelea kwa kusema kuwa kuna kazi inayotarajiwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali maarufu wa uigizaji akiwemo Lulu, Kajala Masanja, Aunt Ezekiel, Dude na wengine wengi.

Leave A Reply