The House of Favourite Newspapers

Wolper Asarenda kwa Wanaume

MKALI wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe amesarenda na kufunguka kuwa, mwanamke yeyote ni vyema akajituma kwa sababu hakuna mwanaume anayehonga kwa sasa.

Akipiga stori na Ijumaa Wikienda, Wolper alisema kuwa, zamani mwanamke alikuwa anashindwa kujitegemea kwa sababu alijua kuna hela atapewa na mwanaume fulani, lakini kwa sasa hiyo haipo kwani wanaume nao wamebana hivyo ni bora wakajituma na kujisimamia mwenyewe kwenye kazi wanazozifanya.

 

“Mambo ya kusubiria hela ya kuhongwa nilishafuta kwenye kichwa changu ndipo nikapata nguvu ya kufanya kazi zangu maana hela za kuhongwa sizitaki kabisa,” alisema Wolper.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa sasa kazi yake ya ushonaji imemfanya kuanza kujulikana hadi nje ya nchi huku akiwandaa wasichana wadogo ili waweze kujitegemea.

 

STORI: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.