The House of Favourite Newspapers

Wolper Atamani Kumpa Penzi Rais

STAA anayejua kupigilia pamba kali ndani ya Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe amefunguka kuwa, anatamani kama ni kutoa penzi lake, basi alitoe kwa Rais yeyote mmojawapo barani Afrika.

Wolper alisema kuwa, anajua wazi penzi lake hilo litakuwa kwenye mikono salama na siyo kwa ‘wadananda’.

Katika mastori ya hapa na pale na Ijumaa Wikienda, Wolper alisema mara nyingi amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao mwishoni wanamsaliti.

Alifunguka kuwa, jambo hilo la kusalitiwa halipendi na linamkera, lakini anaamini akimpa moyo wake wa upendo Rais yeyote Afrika anaona atakuwa salama.

“Unajua ndoto yangu mimi ningependa kutoa penzi langu kwa Rais maana najua kabisa, kwanza atakuwa ananiheshimu na itakuwa ni ngumu sana kunitenda kama wafanyavyo wengine na hapo nitatulia kabisa wala sitakumbuka wanaume wazugaji,” alisema Wolper.

STORI: Imelda Mtema, DAR

Comments are closed.