The House of Favourite Newspapers

WOLPER AUZA GARI ANUNUA MATIRIO YA GAUNI

Jackline Wolper

MUIGIZAJI Jackline Wolper ameamua kuliuza gari lake aina ya Toyota Brevis na kununua ‘matirio’ ya kutengenezea magauni.  

 

Wolper aliiambia Za Motomoto kuwa aliamua kuchukua uamuzi wake huo baada ya kupendezwa na matirio hayo alipokuwa nchini Dubai hivi karibuni.

“Unajua mimi ni fundi cherehani hivyo  nilivyofika nchini Dubai na kuwaona wadada wakipendeza kwa kuvaa magauni kama haya na nilipowaangalia niliona kabisa kuwa nayamudu kuyadizaini.

 

“Nilichoamua kufanya ni kuuza gari yangu na kwenda kununua matirio haya na kutengeneza magauni kadhaa ambayo kama hili na mengine nayauza. Kwa sasa natumia usafiri wa kukodi na hilo kwangu sioni shida,” alisema Wolper ambaye alikutwa na mwandishi akiwa amevaa moja ya gauni aliotumia matirio hayo.

Comments are closed.