The House of Favourite Newspapers

NJEMBA AMFANYIA KITU MBAYA MWANAMKE ALIYEZIRAI, YAMKUTA!

MWANAMME Isrrael Cordero (47) wa Long Branch, Marekani, amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kufanya shambulio la ngono kwa mwanamke” aliyekuwa hajiwezi na akiwa amepoteza fahamu” katika baa moja baada ya kufungwa juzi (Jumanne).

 

“Shambulio hilo liligundulika baada ya Cordero kuwaita polisi siku ya Machi 3, 2017, aliposema alikuwa ameshambuliwa na mwanamke huyo baada ya kufanya ngono waliyokubaliana,” Mwendesha Mashtaka J. Gramiccioni alisema katika taarifa.

 

Lakini video za siri zilinasa tukio zima la shambulio hilo ambapo zilionyesha kwamba mwanamke huyo alikuwa hajiwezi na alikuwa amepoteza fahamu.  Na ilifahamika kwamba wawili hao walikuwa wanajuana. Mahakama ilimkuta mwanamme huyo na makosa sita ya mashambulio ya ngono.

 

Akimhukumu, Jaji  Torregrossa-O’Connor alisema Cordero alikosa huruma na alikuwa amevunja haki ya faragha na heshima ya mhanga huyo. Shane Paugh, mwanasheria wa Cordero, alisema tukio hilo lililompata mteja wake lilikuwa fundisho kwa watu wanaochanganya madawa na ngono.

 

Cordero lazima atumikie asilimia 85 ya hukumu yake ya kifungo hicho, ambacho ni miaka 12 na miezi 9, kabla hajafikiriwa kuachiwa kwa msamaha.  Ni lazima pia asajiliwe kama mtu aliyetenda kosa la ngono kwa mujibu wa Sheria ya Megan.

Comments are closed.