The House of Favourite Newspapers

Yanga inatia huruma Yapigwa na Biashara United bao 1-0

Kikosi cha Yanga

HADI dakika 90 zinamalizika, wachezaji wa Yanga walitoka uwanjani wakiwa hawaamini kitu kufuatia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Biashara United.

 

Mchezo huo uliopigwa Dimba la Karume mjini Musoma, ulihudhuriwa na mashabiki kibao wa Biashara United ambao muda wote walikuwa wakiishangilia timu yao hasa ilipokuwa inamiliki mpira.

 

Biashara kwa sasa inapambana kuhakikisha inabaki ligi kuu kwani kabla ya mechi ya jana ilikuwa nafasi ya tatu kutoka mkiani lakini baada ya ushindi ikakwea hadi nafasi ya 17.

 

Mechi hiyo ilichezwa huku mvua kubwa ikinyesha kuanzia dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na kusababisha wachezaji wa timu zote kuteleza na kuanguka mara kwa mara hali iliyopoteza utamu wa soka.

 

Biashara ilianza kwa kasi mchezo huo ikisaka heshima nyumbani lakini pia kujiondoa kwenye wimbi la kushuka daraja wakati Yanga nao walikuwa hawataki kuona wanaaibishwa na ‘wageni’ kwenye ligi kuu msimu huu.

 

Bao pekee la Biashara lilifungwa na mchezaji Tariq Seif dakika ya tisa baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga ambao walidhani ameotea kisha akaukwamisha wavuni kiulaini mpira na kumuacha kipa Klaus Kindoki akiangukia kulia na mpira ukaenda kushoto.

 

Baada ya bao hilo Yanga walijitahidi mara kadhaa kushambulia lango la Biashara lakini mabeki wao walikuwa imara na kuondosha hatari.

 

ZAHERA ALIA NA MWAMUZI

Baada ya mchezo huo, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alilalamikia maamuzi ya waamuzi waliochezesha mchezo huo wakiongozwa na Danile Warioba wa Mwanza na kwamba ingekuwa amri yake angemfungia kuchezesha soka miaka minne.

“Goli tulilofungwa lilikuwa la kuotea, waamuzi wanashindwa kutafsiri sheria za soka ingekuwa mali yangu ningemfungia miaka minne. Utasikia baada ya mchezo huu TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) watamfungia miezi alikokuwa amekaa na kumtoa kinguvu.

Awali, gari hilo aina ya Coastal liliingia uwanjani likiwa na wachezaji wa Yanga na waliposhuka Jaffar alikuwa amebaki ndani peke yake ndipo mashabiki hao wakaenda kumtoa kinguvu. Hata hivyo kabla hawajafika mbali zaidi, watu wa usalama waliingilia kati ya kumpeleka Jaffar jukwaani kwa kuwa hakuwa sehemu ya wachezaji waliocheza jana dhidi ya Biashara United.

Aidha mchezo huo ulikuwa na fujo za hapa na pale ambapo wakati fulani mashabiki wa Yanga na Biashara walioneakana wakirushiana chupa za maji kabla ya gari la ulinzi ‘washawasha’ kuwaonyeshea ishara ya kuwataka watulie wakanywea na kuendelea kuangalia soka.

miwili,” alisema Zahera.

MASHABIKI BIASHARA WAMVAA KIUNGO YANGA

Mashabiki wa timu ya Biashara United, jana walimfanyia fujo Kiungo wa Yanga, Jaffar Mohammed baada ya kuvamia kwenye gari

Comments are closed.