The House of Favourite Newspapers

‘Yanga SC hii ya sasa itawashangaza wengi’

BAADA ya kucheza na timu zote mbili, Simba na Yanga, Kocha wa Stand United, Amars Niyongabo raia wa Burundi, amesema leo Yanga itawashangaza wengi. Simba na Yanga zitamenyana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

 

Mechi ya mzunguko wa kwanza ilimalizika suluhu. Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyongabo alisema, wengi hawaipi nafasi Yanga kutokana na mwenendo wake wa mechi za hivi karibuni, ila wana kitu cha ziada ambacho kitawashangaza wengi.

 

“Naiheshimu timu ya Yanga, ni timu kubwa na ukitizama kuelekea kwenye mchezo wao wa watani wengi wanasahau kwamba Yanga inaongoza ligi kwa sasa, hivyo sio ya kuibeza hata kidogo, itafanya maajabu ambayo wengi hawatarajii.

 

“Uwezo na kasi yao uwanjani hasa kwa kubadili matokeo, wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri. “Kwa upande wa Simba, kitakachowaponza kama watajiamini kupitiliza baada ya kumfunga Mwarabu itakuwa ngumu kupata matokeo, hivyo wasiibeze Yanga,” alisema Niyongabo.

Comments are closed.