The House of Favourite Newspapers

Yanga Wako Bize Kutafuta Pointi 3 Kwa Azam

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameendelea na mazoezi yao kuhakikisha wanakuwa vizuri kabla ya kuivaa Azam FC keshokutwa Jumamosi.

Yanga wamefanya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakionekana wako tayari kwa mechi hiyo.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa ni kama fainali kwa Yanga ambayo kama itateleza itakuwa imejiweka mbali zaidi dhidi ya watani wake Simba ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba dhidi yao.

 

Comments are closed.