Yanga Yaifunga Mbao FC Bao 1-0, CCM Kirumba

TIMU ya Yanga SC leo Jumanne Oktoba 22, 2019 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom. Bao la Yanga limefungwa na Sadney Urikhob dakika ya 57 kipindi cha pili.
Yanga imefikisha pointi saba ikiwa katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi baada ya kucheza mechi nne. Simba inaongoza Ligi ikiwa na pointi 12 wakiwa na michezo minne, nafasi ya pili ikishikiliwa na Namungo FC wakiwa na pointi 10 wakiwa wamecheza michezo sita.



Comments are closed.