The House of Favourite Newspapers

Yanga Yajipangia Pointi Zao Caf

BAADA ya Yanga kuanza vibaya mi­chuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi na kuburuza mkia wa Kundi D, kaimu kocha mkuu wa kikosi hi­cho, Noel Mwandila raia wa Zambia, ameibuka na kusema wanahitaji pointi 10 ili waingie robo fainali.

 

Yanga ambayo imepangwa Kundi D na timu za USM Alger ya Algeria, Gor Mahia (Kenya) na Rayon Sports kutoka Rwanda, inaburuza mkia katika kundi hilo ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili, imepoteza moja na kutoka sare moja.

 

Katika kundi hilo, USM Alger inaongoza ikiwa na pointi nne, huku Gor Mahia na Rayon zikiwa na pointi mbili. Timu hizo zote zimecheza mechi mbili mpaka sasa, huku zote zikibakiwa na mechi nne za hatua ya makundi.

 

Juzi Jumatano, Yanga ililazimishwa suluhu na Rayon Sports katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, ambapo Mwandila amesema ni lazi­ma wakusanye pointi 10 au zaidi kwa lengo la kusonga hatua inayofuata.

“Sijafurahishwa na ma­tokeo haya kwani matarajio yetu yalikuwa ni kuona tunashinda mchezo huu kutokana na kucheza ny­umbani, kwa bahati mbaya hatukuweza kupata ushindi.

 

“Kilichobaki sasa ni kushinda mchezo ujao wa ugenini na mingine ya ny­umbani iliyobaki, tunataka kufikisha pointi kumi au zaidi ili tuvuke hatua hii, tu­naamini bado tuna nafasi ya kufuzu,” alisema Mwandila.

Stori: Omary Mdosen a Said Ally

Comments are closed.