YANGA YAZINDUA JEZI MPYA DAR (PICHA + VIDEO)

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imetambulisha jezi zake kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya ndani na kimataifa ambazo zimetengezwa na kampuni ya GSM ya Dar es Salaam.
Jezi hizo zimezinduliwa katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam, ambapo zile za rangi ya kijani zitakuwa za nyumbani na zile njano zitakuwa ni za ugenini.

Mtendaji mkuu wa GSM, Eng. Heris Said, amesema kwa mara ya kwanza Tanzania kumezinduliwa jezi bora ambazo hazijawahi kutokea na akawaasa mashabiki wa Yanga kununua jezi halisi.
Yanga itaanza kuzitumia jezi hizo keshokutwa Jumapili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Shabiki wa timu ya Yanga akikabidhiwa jezi.
PICHA NA MUSA MATEJA | GPL


Comments are closed.