The House of Favourite Newspapers

Simba Watembelea Sportpesa Wapatiwa Mil. 150

KAMPUNI ya mchezo wa kubashiri ya Sportpesa Tanzania, hatimaye imekabidhi cheki ya Shilingi Milioni 100 kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2018/19, ambao ulinyakuliwa na timu ya Simba, msimu uliopita huku wakiwapatia pia hundi ya Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kufanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba na Yanga zote zinadhaminiwa na Kampuni ya Sportpesa, ambapo katika mkataba wao hutakiwa kupewa kitita hicho cha Shilingi Milioni 100 kwa kila timu inayochukua ubingwa, na  Simba tangu Simba iingie mkataba na kampuni hiyo, hii ni mara yake ya pili mfululizo ikitwaa kombe hilo na kulamba kitita hicho.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Mkurugenzi wa Udhibiti na Uzalishaji wa Sportpesa, Tarimba Abass, alisema kuwa wanaendelea kujivunia mafanikio ya Simba kutokana na kuendelea kuiwakilisha vyema kampuni hiyo, ambapo msimu uliopita waliwawakilisha vizuri lakini msimu huu wamezidi zaidi hasa baada kufanya vizuri pia kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwa niaba ya Sportpesa Tanzania ninaomba kutumia frusa hii kuipongeza klabu ya Simba kwa kuendelea kutuwakilisha vyema kwa misimu miwili mfululizo.  Hakika hili ni jambo la heshima kwetu kwani wamezidi kuipeperusha bendera ya kampuni yetu kama tulivyokuwa tumetarajia.

“Zaidi ya yote sisi kama kampuni ya Sportpesa Tanzania tumeamua kutoa zawadi ya Shilingi milioni 50 kwa Simba, kutokana na kufanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kwa ujumla wake tumetoa milioni 150, ambapo 100 ni zile za ubingwa wa ligi kuu na 50 za kuingia hatua hiyo ya robo.

“Tutaendelea kuzidhamini klabu zetu kwa kila mafanikio wanayoyapata kwani kufanya kwao vizuri kutaijenga zaidi timu yetu ya taifa kwa kuiletea ushindani zaidi, lakini hata katika klabu zingine nazo zitaendelea kuiga na kutamani kufikia hatua kubwa kama hiyo,” alisema Tarimba.

(PICHA NA MUSA MATEJA | GPL)

SHANGWE La YANGA Wakizindua JEZI Zao RASMI, JANGWANI Kumekucha!

Comments are closed.