The House of Favourite Newspapers

Yemi Alade: Nilimtabiria Nandy Atakuwa Msanii Mkubwa

yemi-fiester-na-snura-na-teknoDAR ES SALAAm: Msanii wa kike maarufu nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla ambaye atakuwa ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta leo Jumamosi, Novemba 5, 2016, Yemi Alade amemsifia msanii wa Bongo, Nandy kwa kudai kuwa alitabiri atakuwa msanii mkubwa.

nandyNandy.

Akimwaga sifa hizo mbele ya waandishi wa habari jana Ijumaa wakati wa kuwatambulisha wasanii watakaotumbuiza kwenye jukwaa la tamasha hilo la aina yake litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders, Yemi Alade ameisifia video mpya ya msanii huyo ‘Nagusagusa’ na kusema kuwa alijua tangu mwanzo muimbaji huyo atakuwa ni msanii mkubwa kwa kuwa alishawahi kumuona kwenye Mashindano ya Kutafuta Vipaji ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.

tekno-milesTekno

Mwanadada Nandy ni msanii mmoja wapo aliyechaguliwa kufanya shoo kwenye tamasha hilo. Wasanii wengine wakubwa watakaokinukisha ni pamoja na Weusi, Maua Sama, Navy Kenzo, Alikiba, Mr Blue, Rayvanny, Darassa, Jay Moe, Barakah The Prince, Bill Nas, Fid Q, Belle 9 na wengine.

bChameleone2Jose Chameleon

Mbali na Yemi Alade, wasanii wengine maarufu wa nje ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo ni pamoja na Tekno wa Nigeria na Jose Chameleon wa Uganda.

Comments are closed.