Yusuph Mlela Amtolea Povu Nay wa Mitego

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela.

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi staa wa Bongo Fleva, Nay Wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii  wa filamu nchini.

@naytrueboy Duh!

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni matahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe hakina tija na mantiki yoyote.

Kutokana na maneno ya Nay wa Mitego kumepelekea kumtolea Mlela kumtolea uvivu kupitia akaunti yake ya Instagram na kusema haya;

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano” alisema Mlela

Staa wa Bongo Fleva, Nay Wa Mitego.

Mbali na hapo msanii huyo pia ameomba mpambano na Nay wazichape

“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela

Wabongo Wasiopenda kuambiwa Ukweli.? #Wapo

A post shared by NayTrueboy (@naytrueboy) on


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment