The House of Favourite Newspapers

ZABIBU KIBA MJAMZITO?

Zabibu Kiba

DADA wa msanii wa Bongo Fleva, Ally Saleh Kiba ‘Alikiba’, Zabibu Kiba amedaiwa kunasa ujauzito na kwamba tayari kitumbo kimeanza kuchomoza. 

 

Picha ya Zabibu ambaye hivi karibuni aliolewa na mwanandinga Abdi Banda ilianza kusambaa kupitia mtandao wake wa WhatsApp ambapo wapenda ubuyu waliichukua picha hiyo na kuanza kuijadili mitandaoni.

 

Baada ya picha hiyo kuzua gumzo, mwishoni mwa wiki iliyopita Amani lilimtafuta mrembo huyo ambaye amehamishia makazi yake ya kudumu nchini Afrika Kusini kwa mumewe Abdi anayesakata kandanda nchini humo katika timu ya Baroka ambapo alipopatikana alikanusha madai hayo na kudai kuwa amenenepa tu. “Hahaha jamani sina kitumbo ni unene tu huu,” alisema Zabibu

STORI: Memorise Richard, Amani

Comments are closed.