The House of Favourite Newspapers

Zahera Aitaja Mipango ya Ubingwa Yanga SC

Mwinyi Zahera

KOCHA wa Yanga, Mkongo, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kama waamuzi watabadilika na kuchezesha kwa kufuata sheria basi timu yake itaendelea kufanya vyema hasa katika mechi zake za mikoani.

 

Hayo yamekuja siku chache baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Stand United kwa kufungwa bao 1-0 ambao ulipigwa katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Akizungumza na Championi, Zahera alisema kuwa hajakata tamaa, anaamini timu yake itaendelea kufanya vizuri kama waamuzi wataamua kubadilika.

 

Kocha huyo alisema kuwa mfano mchezo wa Stand, waamuzi ndiyo walikuwa tatizo ndiyo maana hata wao walishindwa kufanya vyema. “Unajua kama waamuzi wetu watabadilika, timu yetu itakuwa na nafasi ya kuendelea kufanya vizuri, hasa mechi zetu za mkoani ambazo kwa sasa ni nyingi, sababu ndiyo wanaochangia kuvuruga michezo.

 

“Lakini mipango yetu haijaharibika, tutaendelea kupambana kuona timu yetu inafanikiwa kufanya vizuri na kuendelea kuwa katika nafasi nzuri,” alisema Zahera.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.