The House of Favourite Newspapers

ZAHERA: Msitetemeke Waacheni Waende, Timu Itakaa Vizuri – Video

WAKATI Timu ya Yanga ikitarajiwa kutua uwanjani leo Jumamosi, Machi 30, 2019 kukipiga na Alliance FC, mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho la Azam katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, kocha mkuu wa Yanga, Raia wa DRC, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana hofu na mchezo huo licha ya kukosekana kwa nyota wake wa kikosi cha kwanza akiwemo Ibrahim Ajibu.

 

Akizungumzia kuhusu mchezo huo huku timu yake ikiwakosa wacheza sita wa kikosi cha kwanza, Zahera amesema; “Juma Abdul, Mohamed Banka, Haji Mwinyi, Ibrahim Ajibu hawa wamebaki Dar, Gadiel Michael yeye amekwenda Afrika kusini kwa ajili ya majaribio, Ramadhan Kabwili yupo kwnye Timu ya Taifa chini ya miaka 20.

 

“Sina mashaka, nipo tayari kwa mchezo wangu wa kesho na nimewaambia wachezaji wangu wapambane na tutapata matokeo kila kitu kinawezekana, kama mchezaji anataka kuondoka kwenye klabu akatafute maisha kwingine, mwacheni ande wala msitetemeke, Yanga ni timu kubwa na itakaa vizuri tu” amesema Zahera.

 

VIDEO: MSIKIE ZAHERA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.