The House of Favourite Newspapers

ZAMBI ATAJA UTAJIRI WA LINDI KWENYE UWEKEZAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (kulia), akimkaribisha Godfrey Zambi ofisini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi  amesema mkoa wake una utajiri mkubwa katika sekta ya uwekezaji na una fursa kwa biashara na amekaribisha wawekezaji wanaotaka kuweza katika miradi mbalimbali kwenye mkoani humo.

Akizungumza na Global Tv on line Jumatatu iliyopita alipotembelea ofisi za Global Group, Zambi alisema mkutano wa fursa za uwekezaji utafanyika mkoani Lindi, Machi 26 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambapo pia atazindua kiwanda cha kusaga muhogo.

RC Zambi akisaini katika kitabu cha wageni ofisini hapo.

Alisema mama Samia ataanza ziara mkoani Lindi Machi 22 hadi 28 mwaka huu na amewakaribisha wawekezaji kwenda kwenye mkoa wake kwa kuwa Dar es Salaam na Pwani kiuwekezaji, kumejaa. Zambi alizitaja baadhi ya fursa zinazohitaji wawekezaji mkoani Lindi kuwa ni pamoja na viwanja vya chumvi, madini, zao la ufuta na korosho.

Shigongo akimkaribisha Zambi ofisini kwake.

Mkuu huyo wa mkoa aliendelea kutaja fursa zingine zinazohitaji wawekezaji kuwa ni madini na gesi, makaa ya mawe, ambazo alisema ni maliasili zinazopatikana kwa wingi mkoani Lindi.

Zambi alisema mkoa wake pia ni sehemu ya Pori la Akiba la Selous ambapo mkoa huo umechukua asilimia 25 ya mbuga hiyo iliyosambaa katika kanda nane nchini ambapo kanda ya kusini pekee ina ukubwa wa kilomita za mraba 7,022.

Picha ya pamoja.

Fursa nyingine aliyoitaja ni uwekezaji katika viwanda vya nyama katika mkoa huo ambao awali ulikuwa na idadi ndogo sana ya mifugo lakini kwa sasa ni moja kati ya mikoa inayoongoza kwa ufugaji. Zambi amewakaribisha wawekezaji kufanya uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo.

Stori na Elvan Stambuli, Picha na Musa Mateja | Global Publishers.

Comments are closed.