The House of Favourite Newspapers

ZARI AMUIGA WEMA

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

WAKATI Wema Sepetu akishikilia jina la Tanzania Sweetheart, mrembo wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ naye ameamua kumuiga kwa kujiita Uganda’s Sweetheart. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Snapchat, Zari aliweka picha yake na kuambatanisha na maneno hayo ya Uganda’s Sweetheart hali ambayo ilisababisha gumzo mitandaoni.

“Mh! Bi dada naye kaona amuige Wema kwa kujipa jina la Sweetheart, makubwa,” alichangia mmoja wa wadau wa mtandao wa Instagram baada ya kipande hicho cha picha kusambaa. Hata hivyo, Zari hakueleza chochote licha ya wadau wengi mitandaoni kusema kwamba amemuiga Wema ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitumia jina la Tanzania Sweetheart.

Comments are closed.