The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zimbabwe Yaihoji Vatican Ukosoaji wa Maaskofu

0

SERIKALI ya Zimbabwe imewasiliana na mwakilishi wa Vatican, Askofu Mkuu Marek Zalewski, kupata maelezo juu ya ukosoaji wa maaskofu wa Kikatoliki dhidi yake.

 

Hivi karibuni maaskofu hao walitoa barua ya kitume wakielezea ufisadi, umaskini na ukiukaji wa haki za binadamu vilivyokithiri nchini humo. Walitoa wito wa kutatuliwa haraka wa matatizo ya kiuchumi na kisiasa nchini humo.

 

Waziri wa sheria, Ziyambi Ziyambi, anasema serikali inataka kujua iwapo maaskofu hao walizungumza kwa niaba ya serikali ya Vatican.

 

“Serikali inataka kuzungumza na Vatican kuelewa iwapo taarifa ya aina hiyo inaonyesha msimamo rasmi wa mkuu wa Vatican kuelekea utawala wa Zimbabwe au haya ni maoni ya watu?” alisema.

 

Ziyambi amesema kuwa Waziri wa Mambo ya nje Sibusiso Moyo atakutana na mwakilishi wa Vatican nchini humo.

Leave A Reply