The House of Favourite Newspapers

Zimebaki Siku 15 Mshindi Wa Milioni 100/- Kupatikana Kupitia Kamata Mpunga

Zikiwa zimebakia siku 15 kwa promosheni ya”Kamata Mpunga”kuisha na mshindi mmoja wa droo ya mwisho atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 100. Leo hii  mkazi wa Moshi mjini Hassan Ochieng amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 20/= na Mkazi wa singida mjini ambaye ni muuza mitumba Bw. Aman Manyenye amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5/= pamoja na Joseph Machima,Mkazi wa Sengerema Mkoa wa Mwanza.

“Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ametoa wito kwa wateja wa kampuni hiyo na watanzania wote kwa ujumla ambao hawajajiunga na mtandao huo waweze kujiunga na kuchangamkia frusa hii yakipekee kabisa kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/- na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na mwisho wa mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/=

Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi  300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”.

maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi.

Kuna wateja wengine hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni hii wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa kiasi cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila watakuwa wameingizwa kwa droo moja kwa moja.

Mpaka sasa jumla ya washindi 327 wamejinyakulia fedha mbalimbali tangu kuanza kwa promosheni hii.

Washindi 297 wamejishindia Milioni mojamoja kila mmoja

Washindi 18 wa wiki wamejishindia shilingi Milion 5/5 kila mmoja

 Pia washindi 4 wameondoka na  kitita cha shilingi Milioni 20/-

Mwisho

Comments are closed.