The House of Favourite Newspapers

Zuma Kutolewa Gerezani?

0

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anaweza kutolewa gerezani kwa dharura ili aweze kuhudhuria mazishi ya kaka yake, Michael Zuma.

 

Hata hivyo, hakuna majibu kutoka serikalini, lakini baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kwamba, mawakili wa familia ya Zuma wamewasilisha ombi la dharura la kumwachilia Rais huyo wa zamani amuage kaka yake.

 

“Wiki hii mazishi yatafanyika na tunatumai ndugu yangu atapewa ruhusa ya kushiriki mazishi kabla ya hapo, Yeye ni mzee aliyebaki na marehemu ni rafiki  yake,” anasema msemaji wa familia Khanya Zuma.

 

Vyombo hivyo vya habari vimeripoti kuwa, Michael Zuma alifariki dunia wiki iliyopita wakati Zuma akitumikia kifungo cha miezi 15 jela katika Gereza la KZN baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya Katiba kwa kupuuza amri ya mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Rais.

Stori: Sifael Paul

Leave A Reply