The House of Favourite Newspapers

Baba Yoyoo Yamkuta Akichafua Mazingira

0

baba yoyoo masai kikojozi (4) Baba Yoyoo akimgombeza mwenzake baada ya kuchafua mazingira.

KELVIN SHAYO NA HILARY DAUDI, RISASI mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Mmasai mmoja mwanaume, ambaye sehemu za mijini wanafahamika kama akina Baba Yoyoo, hivi karibuni yalimkuta ya kumkuta baada ya kukutwa akichafua mazingira maeneo ya Sinza Kijiweni, Kinondoni jijini Dar, baada ya kutaitiwa na viongozi wa mtaa, OFM ilishuhudia.

baba yoyoo masai kikojozi (5)Majira ya saa 2.13 usiku, makamanda wa Kitengo Maalum cha Kufichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, wakiwa katika mizunguko yao ya kawaida,  walisikia vurumai zikitokea upande wa pili, na walipotupia macho, waliona mkusanyiko ukiwa umemzunguka Mmasai huyo.

baba yoyoo masai kikojozi (3)Baada ya kusogea OFM ikaambiwa kuwa Baraka Mollel alikutwa akikojoa katika mtaro wa maji machavu, kitendo ambacho ni kosa kwani anachafua mazingira. Aliyeongoza ukamatwaji huo, alitajwa kwa jina moja la Mubaraka aliyejitambulisha kuwa ni kiongozi wa mtaa huo.

baba yoyoo masai kikojozi (2)Mmasai huyo alitakiwa kulipa faini ya shilingi elfu 50, ambazo hakuwa nazo, jambo lililomfanya ajitetee huku akilia na kuomba msamaha. Mmoja wa watu waliokusanyika, alikuwa ni Mmasai aliyekataa kutaja jina lake, aliyemtosa mwenzake kwa kumgongagonga na fimbo yake kichwani, akidai ameidhalilisha jamii yao.

baba yoyoo masai kikojozi (1)Hata hivyo, kilio na maneno yake ya kuomba msamaha, yalisababisha baadhi ya mashuhuda kuwasihi viongozi hao kumsamehe, wakisema kwake ni fundisho ambalo pia wanapaswa kulipata watu wengine. Mollel alisamehewa na kupewa onyo la kutorudia tena kitendo hicho katika eneo lolote jijini Dar es Salaam.

Licha ya Mmasai huyo, katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, baadhi ya wakazi wasio wazalendo, wamekuwa wakitupa mizigo ya takataka katikati ya barabara nyakati za usiku na kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa mchana.

OFM kinaungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amekuwa akisisitiza usafi na ulindwaji wa mazingira, kitu ambacho baadhi ya wakazi wamekuwa hawakizingatii, hasa nyakati za usiku. OFM inaahidi kutembelea na kupata picha za wachafuzi wa mazingira kote jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply