The House of Favourite Newspapers

Darassa Awaombea Kwa Mungu Waliotaka Kusababisha Ajali Wakicheza Wimbo Wake Kwenye Gari

darassa-muzikiRAPA anayekimbiza kwenye game ya Bongofleva kwa sasa, Darassa huku akifanya vyema na single ya wimbo wake mpya ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ile video iliyosambaa mitandaoni ikionesha vijana wakicheza wimbo wake huku dereva akiacha gari likiendelea kuseleleka lenyewe huko Itigi, mkoani Singida.

Taarifa iliyopo ni kwamba, vijana hao wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida linawashikilia kwa mahojiano ili sheria ichukue mkondo wake.

MUZIKI YA DARASSA YAWAPONZA VIJANA HAWA WALIOTAKA KUSABABISHA AJALI

 

Kutokana na tukio hilo, Darassa ameamua kutoa mawazo yake kuhusiana na kitendo hicho, akitumia account yake ya instagram Darassa ameonesha kuguswa na vijana hao na kuandika haya:

“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie 🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“

 Darassa ft Ben Pol – Muziki ( Official Music Video )

Comments are closed.