The House of Favourite Newspapers

Efm Radio, Vodacom kuja tena na muziki mnene

0

1

Meneja wa Efm, Dennis Ssebo (kulia) akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).

2

Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzungumza na wanahabari.

3

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom, Nandi Mwiyombela (kushoto) akizungumza jambo.

Stori: Hilaly Daudi

IKIWA ni mara nyingine tena Kituo cha Radio cha Efm chini ya udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imeandaa Tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama ’Muziki Mnene’ linalotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 27, mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari katika Ofisi za Efm zilizoko Kawe-Mikocheni jijini Dar es Salaam, Meneja wa Efm, Dennis Ssebo alisema kuwa lengo kubwa ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na Mkoa wa Pwani, kwa namna walivyoipokea Efm Radio na kushirikiana nao hadi kufikia sasa.

Amesema tamasha la muziki mnene mwaka huu litafanyika kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu ambapo muziki utapigwa katika baa 12 za jiji la Dar na Pwani likiwa limebeba kauli mbiu ya ”TUNASEPA NA KIJIJI” ikiwa na maana kuwa, kila wiki Efm itaweka kambi katika kijiji kimoja ama eneo moja kwa muda wa siku nne.

Aidha Ssebo aliongeza kuwa, muziki mnene mwaka huu utaenda sanjari na kampeni ijulikanayo ‘NJE NDANI’ ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika.

Alivitaja vipindi hivyo kuwa ni: Uhondo (Siku ya Jumatano), Sports Headquarters (Alhamisi), Joto la Asubuhi (Ijumaa) pamoja na Funga Mtaa (Jumamosi) na burudani kutoka kwa RDJ’s wa Efm.

Pia kwa muda wa asubuhi kutakuwa na Jogging, Singeli, Michano kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki, mpira wa miguu kati ya Timu ya Efm na Timu za Maventerans wa eneo husika.

Leave A Reply